Anasema mwanamke: Niliolewa na mmoja wa mwanaume ambaye ni ktk jirani zangu. Na watu Wote wa ukoo wake walikuwa matajiri – walimiliki biashara, maduka, na nyumba kubwa za kifahari.
Lakini familia yake mwenyewe ilikuwa masikini sana, hawakuwa na biashara wala maduka kama ndugu zake wengine.
Cha kuhuzunisha ni kwamba ndugu zake hawakuwa na huruma naye, hawakumjali wala kumhesabu kuwa sehemu ya familia. Walimchukulia kama mlinzi tu, si zaidi.
Siku moja aliugua sana na hakuweza kwenda kazini kwa siku tatu. Walikata mshahara wake – lakini hakulalamika wala kuwaomba msaada kwa kuwa wao ni wa familia yake.
Aliendelea na kazi kama vile hakuna kilichotokea.
Nilikuwa nikihuzunika mno kwa jinsi mume wangu alivyodhalilishwa na kudharauliwa. Nilitamani aache kazi ile na atafute kazi nyingine kokote.
Alidumu katika kazi hiyo kwa miaka mitano tangu tulipooana.
Siku moja nilihisi uchovu na maumivu. Nilipogundua kuwa mjamzito, nilifurahi sana – kwa sababu nilikuwa nimesubiri kwa miaka mingi.
Nilipomwambia mume wangu, alifurahi sana mpaka akapagawa, lakini ghafla uso wake ukabadilika na kuwa wa huzuni.
Nikamuuliza: “Kwanini umebadilika uso, mpenzi wangu?”
Akasema: “Mtoto wetu anakaribia kuja, lakini sina pesa ya kumnunulia nguo au mahitaji yake.”
Nikamwambia: “Usijali, riziki yake italetwa na Yule anayewaruzuku ndege angani hawezi kushindwa kuturuzuku sisi duniani.”
Maneno haya yalimpa faraja, na furaha ikamrudia.
Zilipofika siku za kujifungua, nilianza kuhisi maumivu makali. Mume wangu akamleta muuguzi nyumbani. Baada ya saa na nusu za kujaribu kujifungua, muuguzi alisema haiwezekani kujifungua kawaida – ni lazima niende hospitali.
Mume wangu aliogopa sana, na hatukuwa na hata senti moja nyumbani.
Akaenda kutafuta msaada – lakini akarudi mikono mitupu.
Nikamuambia asijitie presha wala asijisumbue. Nilijifungia ndani nikiwa kimya ili nisisikiwe sauti yangu kwa uchungu ninaopitia, nikajikaza. Lakini maumivu yalikuwa makali mno.
Hakuweza kuvumilia kuona hali ile, akaondoka mbio nyumbani – nikaogopa kwamba ameenda kwa jamaa zake kuwaomba msaada. Na kweli – ndivyo alivyofanya.
Alirudi baada ya muda mfupi, macho yakiwa yanamwaga machozi – nikajua wamefunga milango yao na kumkataa.
Nilimuomba Mungu kuchukua roho yangu kuliko kuona machozi ya mume wangu kwa huzuni na fedheha.
Lakini si muda mrefu, hali yangu ikatulia na nikajifungua salama – mtoto wa kike.
Muuguzi alisubiri malipo. Mume wangu akamwambia: “Naapa kuwa malipo yako ni deni shingoni mwangu – nitakulipa mara nitakapopata pesa.”
Muuguzi alikubali kwa huruma na akaondoka.
Kisha nikamuomba mume wangu achane baadhi ya nguo, tukamfunika mtoto wetu kwao vitambaa kwa sababu hatukuwa na hata kipande cha nguo kwa ajili yake.
Nilipomuuliza alikokwenda mara ya mwisho, alisimulia:
Alikwenda kwa ndugu zake kazini. Alikutana na mdogo wao, akamwomba pesa kama mkopo kutoka kwenye mshahara wake. Akajibiwa: “Siwezi kukusaidia – nenda kwa msimamizi wa fedha.”
Msimamizi naye alikataa kwa kusema hawezi kutoa pesa bila idhini ya mkurugenzi.
Akamtafuta mkurugenzi, lakini akaambiwa ametoka muda huo huo. Alimkimbilia nje, akampigia kelele: “Subiri!” lakini hakusimama.
Alirudi ndani akiwa amevunjika moyo, akawaomba tena kwa unyenyekevu, lakini hakuna aliyemsaidia. Aliondoka akiwa amenyongeka mwili wake dhaifu na machozi yakimbubujika
Nikamwambia: “Usijali, mpenzi wangu – nimejifungua salama, Alhamdulillah.”
Kesho yake alikataa kurudi kazini na akaenda sokoni kutafuta kazi.
Baada ya saa nne alirudi na vyakula vya kila aina, nguo, soksi, na mahitaji yote ya mtoto wetu.
Alikuwa na furaha kama mtu aliyepata usiku wa Lailatul-Qadr.
Nilipomuuliza alipataje kazi au pesa, akanisimulia:
Alienda sokoni bila mafanikio. Kisha akakutana na rafiki wa zamani aliyekuwa mfanyabiashara wa mboga.
Akamweleza hali yake na alivyofukuzwa na jamaa zake bila msaada. Rafiki yake alighadhibika na kusema: “La hawla – kama ungekuja kwangu, ningekupa hata roho yangu, si pesa tu.”
Akamkabidhi kalamu na daftari na kumuajiri kuandika idadi ya mizigo inayosafirishwa kwa wateja.
Baada ya kazi kumalizika, alimpeleka dukani, akanunua nguo na mahitaji yote ya mtoto, akampeleka nyumbani, na kumuwekea pesa mfukoni.
Akamwambia: “Nitakuona kesho asubuhi.”
Kesho yake alirudi na vyakula na pesa, na akasema: “Hii tumpe muuguzi.”
Nilipompelekea pesa, muuguzi alikataa kuzipokea huku akilia.
Akasema: “Niliwaacha usiku ule nikiwa nimeacha malipo kwa ajili ya Allah. Nilificha machozi yangu kwa uchungu niliouona.
Niliporudi nyumbani, nilipigiwa simu na namba isiyojulikana – ilikuwa hospitali kubwa ambayo niliwahi kuomba kazi miaka minne iliyopita.
Waliniita na kuniambia nimeajiriwa – sasa mimi ni daktari wa uzazi pale!”
Mwanamke anasema: “Nilishangaa kwa ukarimu wa Mungu – alipoacha malipo yake kwa ajili ya Allah, Mungu alimtunuku na kuzitimiza ndoto zake.”
Niliporudi nyumbani, nilimwambia mume wangu.
Akanishangaza kwa kuniambia tujiandae kwa sababu tutahamia mjini.
Nilipomuuliza sababu, akasema: “Rafiki yangu amenitaka nihamie mjini, atanitumia matunda na mboga niwauzie wateja.”
Tukaandaa mizigo, tukahamia mjini, tukaishi katika nyumba kubwa. Hapo maisha yalianza kutunukia na kuwa mazuri– kila siku hali ilizidi kuwa bora.
Baada ya miaka mitatu, mume wangu akawa mfanyabiashara mkubwa na tajiri, akiwa na biashara yake binafsi.
Na maisha yetu yakabadilika kwa neema ya Allah na subira yetu katika wakati wa shida.
Tuambie umepata funzo gani
Sufian Mzimbiri

Comments
Post a Comment